SAMATTA ATANGAZA KUREJEA SIMBA
Straika tegemo katika timu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji, Mbwana Samatta, amesema kuwa endapo atamaliza harakati za maisha yake ya soka atarejea Tanzania kuungana na Simba."Wachezaji wengi wakubwa wanapokaribia kustaafu soka hurudi kwenye vilabu vyao vya zamani ambavyo viliwatoa."Nilikuwa mchezaji wa Simba zamani, hata nitakaporudi baadaye nafikiri nafasi ya kwanza itakuwa kwa Simba kwa sababu niliwahi kuitumikia...
EXCLUSIVE: USAJILI WA BIGIRIMANA WAZUA MSALA YANGA, APR KUCHUKA HATUA ZA KISHERIA
Katibu Mkuu wa APR ya Rwanda Adolphe Kalisa, amefunguka kwa kusema kuwa ameshangazwa na Yanga kwa kumsajili mchezaji wake Issa Birigimana bila kufuata taratibu.Kalisa ameeleza kuwa ameshangazwa na klabu kubwa kama Yanga kufanya maamuzi hayo ili hali mchezaji huyo akiwa bado hajamaliza mkataba wake na APR.Yanga umemtangaza Birigimana kuwa mchezaji wake kwa kusaini mkataba wa miak miwili utakaomalizika mwaka...
Salimu Aiyee na kiboko ya Simba Sc wapo mtegoni.
Kagera Sugar na Mwadui Fc zimeingia katika hatua ya mtoano dhidi ya timu za ligi daraja la kwanza ili kuamua nani atabaki au atapanda Ligi Kuu. Salimu Aiyee ni mfungaji bora kwa wazawa, lakini timu yake ipo hatarini kushuka daraja.Tazama ratiba yao hapa chini, na endelea kufuatilia kandanda kujua ni timu zipi zitapanda.Timu mbili zinasubiriwa kuungana na...
TPL NDO ISHAISHA HIVYO, HIYO RATIBA YA FA INATISHA
BINGWA ndo kama alivyoshinda na Ligi Kuu Bara imemalizika huku timu nyingi zikiwa zimeambulia maumivu makubwa msimu huu.Ilikuwa ni aina moja ya ligi iliyokuwa na ushindani kwa timu chache ambazo zilikuwa zinashiriki ligi hali iliyopoteza ule mvuto na msisimko ambao ulianza awali.Kukosekana kwa mdhamini kumeziminya klabu nyingi na kufanya uendeshaji kuwa mikononi mwa viongozi wenyewe huku wachezaji wakitumia nguvu...
BEKI SIMBA ASAINI YANGA
Uongozi wa klabu ya Yanga umemalizana na beki Lamine Moro kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.Moro ambaye ni raia wa Ghana, ambaye aliwahi kuja Simba kufanyiwa majaribio kipindi cha michuano ya SportPesa CUP, amefikia mwafaka kwa kusajiliwa na Yanga.Beki huyo sasa atakuwa Jangwani mpaka mwaka 2021 akiihudumia timu hiyo ambayo ni bingwa wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.Usajili huo...
YALIYOTOKEA MSIMU HUU YASIJIRUDIE KESHO, WACHEZAJI WAFUNDISHE ‘FAIR PLAY’ UWANJANI
LIGI Kuu Bara imeisha kiubishi kwa kuwa tumeshuhudia namna ilivyokuwa inakwenda kwa mwendo wa kuchechemea ila mwisho wa siku mshindi kapatikana.Simba anapaswa pongezi kwa kutetea ubingwa wake msimu huu kwani haikuwa rahisi kufikia malengo ambayo amejiwekea hivyo ni muda mwingine mzuri kwake kujipanga kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.Msimu huu alifanya vizuri kwa kutinga hatua ya robo...
YANGA KUMALIZANA NA BEKI KISIKI WA KMC
IMEEELEZWA kwamba uongozi wa Yanga umeanza mazungumzo na beki wa kikosi cha KMC, Ally Ally 'Mwarabu' ili kupata saini yake msimu ujao.Mwarabu amekuwa kiongozi ndani ya KMC na kuifanya safu ya ulinzi kuwa kisiki kwani KMC imekuwa ni namba moja kwenye timu zilizotoa sare nyingi ikiwa imefanya hivyo mara 16 msimu huu.Habari zimeelezwa kuwa Yanga tayari wamefikia sehemu nzuri...
ALLIANCE FC KUIFUMUA SIMBA NA YANGA
UONGOZI wa Alliance FC ya mkoani Mwanza umesema kuwa msimu ujao lazima wawe moto hasa kwa kuwapata wachezaji wenye uzoefu watakoongeza nguvu kwenye kikosi chao.Alliance walianza kwa kusuasua msimu huu kabla ya kufanya maboresho kwenye kikosi chao kwa kuleta wachezaji wenye uzoefu pamoja na mabadiliko ya benchi la ufundi.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Alliance, Jackson Mwafulango amesema...
MAURIZIO SARRI KUIBUKIA JUVENTUS
KOCHA Maurizio Sarri, ambaye ametwaa kombe la Europa League msimu huu akiwa na Chelsea, inasemekana ameshafikia muafaka na Juventus kwa ajili ya kuinoa timu hiyo kwa msimu ujao wa 2019/20.Juventus inataka kumchukua Sarri kutoka Chelsea ili kuchukua nafasi ya Massimiliano Allegri, ambaye anaondoka mwishoni mwa msimu huu.Sarri amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa kuinoa Chelsea, ambayo haijaweka wazi...