IFANYE EID YAKO KUWA TAMU KWA KUSHIKILIA ODDS ZENYE UJAZO KUTOKA MERIDIANBET…
Ligi mbalimbali Duniani kuendelea wikendi hii huku kila timu ikihitaji kusaka pointi 3 muhimu ili kusalia kwenye ligi, wengine wakipambania Ubingwa na wengine wakipambani kusalia kwenye ligi. EPL, Bundesliga, NBC, Serie A, Laliga Ligue 1 hizo ni zile kubwa duniani lakini pia kuna zingine kutoka nchini mbalimbali zitapigwa. EPL kurindima katika viwanja mbalimbali huku nafasi ya kuwania Ubingwa ikionekana kubaki...
SIMBA SC WAPANGUA JANJA YA WYDAD KUTAKA KUSHITAKI CAF ENDAPO WATAFUNGWA LEO…
Uongozi wa Simba umeshitukia mbinu za wapinzani wao Wydad Casablanca ya nchini Morocco kuwatoa mchezoni huku wakielekeza akili na nguvu zao katika mchezo huo watakapokutana. Timu hizo zinatarajiwa kuvaana leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Wydad Casablanca mara baada ya kutua walilalamikia kupewa...
MBRAZILI;- MECHI NA WYDAD NILISHAIMALIZA TOKA SIKU NAJIUNGA SIMBA SC…
Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema kikosi chake kipo tayari kuwakabili mabingwa wa Morocco, Wydad Casablanca katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika katika dimba la Benjamin Mkapa, leo Jumamosi (April 22). Simba SC itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi...
BAADA YA KUONA WANIGERIA WANAVYOWEWESEKA….MANARA AIPELEKA YANGA MBELE KWA MBELE CAF…
Mchezaji wa zamani wa Yanga SC Sunday Manara amesema Yanga wana faida kubwa ya kufuzu hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga SC inaanzia ugenini kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Rivers United ya Nigeria, mchezo utakaopigwa kesho Jumapili Manara ambaye ni mchezaji mwenye rekodi kubwa Tanzania amesema wakati walipokuwa wakicheza kimataifa...
SALIM NA CHAMA WAPEWA KAZI MAALUM LEO….MBRAZILI AKESHA NA ONYANGO…
KIKOSI cha Simba SC kina dakika 90 za kuhakikisha inazitumia vizuri katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya kurudiana Aprili 28 ugenini. Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira 'Robertinho' amekaa na nyota wa timu hiyo, beki wa kati, Joash Onyango na...
YANGA SC WAANZA KUKICHAFUA NIGERIA….MORRISON NA WENZAKE WATOA MSIMAMO…
YANGA SC imetua na kuanza mazoezi Nigeria kwenye mji wa Uyo ambako mchezo wao utachezwa Jumapili mchana dhidi ya Rivers, lakini mastaa wa Jangwani wametoa msimamo mzito kwamba ushindi ni muhimu na Fiston Mayele amesema yupo fiti. Yanga SC itachezea kwenye uwanja wa Godwill Akpabio, ambao wenyeji wao Rivers wanaona kama ni faida kwa wapinzani kutokana na ubora wake wa...
ALLY SALIM AULA SIMBA SC…ASAINI MKATABA MNONO….MSHAHARA KAMA WA FEI TOTO…
KIPA namba tatu wa Simba SC, Ally Salim amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu baada ya kuonyesha kiwango kizuri dhidi ya Yanga, timu yake ikishinda mabao 2-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa. Na habari mpya ni kwamba hata mechi leo Jumamosi dhidi ya Wydad Casablanca, Salim ana nafasi kubwa ya kusimama langoni kwani Aishi Manula bado hajakaa sawa na Beno Kakolanya...
MWADUKE :- MECHI YA LEO NA WYDAD…SIMBA SC WACHEZE KAMA WALIVYOCHEZA NA YANGA…
Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Ramadhani Mbwaduke amesema kuwa Simba SC wanayo nafasi ya kushinda katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC. Mbwaduke amesema kuwa hayo yanawezekana iwapo kocha wa Simba SC, Robertinho atafanya homework yake vizuri kwa Wydad kwani mbinu wanayotumia ni kama anayotumia Kocha Nabi wa...
KUELEKEA MECHI YA LEO….RUNGU LA CAF LAIPA AHUENI SIMBA SC…MFUNGAJI WA WYDAD AZUIWA…
HII ni habari njema kwa Simba SC kwamba wapinzani wao Wydad Casablanca ambao tayari wapo Dar es Salaam watakosa huduma ya mshambuliaji wao matata , Bouly Junior ambaye ana kadi tatu za njano. Atakuwa jukwaani tu akifuatilia mechi ya leo Jumamosi jioni. Kukosekana kwa Junior bila shaka ni habari njema kwao kwa sababu mshambuliaji huyo ndiye kinara wa kuweka wavuni...
MANULA NDIO BASI TENA SIMBA SC….KUKOSA MECHI ZOTE ZILIZOBAKI…LEO NI BENO AU ALLY TENA….
MIKOBA ya kipa namba moja wa Simba SC, Aishi Manula kocha wa timu hiyo Roberto Oliveira ataamua ampe Beno Kakolanya ama Ally Salim, robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Wanamsimbazi wakicheza dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco. Ipo hivil; Manula hatakuwepo kabisa kwenye mpango wa Simba kwenye mechi zilizosalia msimu huu, kulingana na tatizo lake la nyonga, benchi la...