MO AMEWASIKIA…USAJILI WA SIMBA UMAFIA MTUPU…WAANZA NA MASHINE HIZI TATU ZA KAZI…
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la Championi la leo Ijumaa.
SIMBA YALETA KOCHA MRENO….NI BOSI WA MGUNDA…KUJA NA MAFUNDI WAWILI..
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la MwanaSpoti la leo Ijumaa.
BAADA YA KUUWASHA MOTO MORROCO…JINA LA OPAH LATUA RASMI CAF…HISTORIA YAWEKWA…
Nahodha na Mshambulaiji wa Simba Queens Opah Clement, ametajwa kwenye kikosi bora cha Afrika mwaka 2022 kilichotangazwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’. Opah ametajwa kwenye kikosi hicho, baada ya kumalizika kwa Michuano hiyo nchini Morocco na wenyeji ASFAR Rabat kutwaa ubingwa wakiichapa Mamelodi Sundows Ladies ya Afrika Kusini 4-0. Mshambuliaji huyo aliifungia Simba SC mabao mawili kwenye Michuano hiyo,...
PAMOJA NA KUWAFUNGIA MAGOLI 5, CHAMA LA MSUVA HUKO UARABUNI TIA MAJI TIA MAJI AISEE…
LICHA ya kwamba chama lake, Al-Qadsiah FC halijauanza vizuri msimu huu wa Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia, Mtanzania, Simon Msuva anaamini wanaweza kumaliza kwa kishindo huku wakipanda daraja. Kabla ya mchezo wa juzi, Jumatatu ambao Al-Qadsiah FC ilikuwa nyumbani katika Uwanja wao wa Prince Saud bin Jalawi, walikuwa wakishika nafasi ya 13 kwenye msimamo wenye timu 18 wakiwa na...
FT: YANGA SC 4-1 SINGIDA BIG STAR….MAYELE AFANYA YAKE…KAGERE AENDELEA KUWACHOVYA YANGA…
Yanga Sc wamerejea kileleni kwa kuiadhibu Singida Big Star kwa mabao 4-1 kwenye ligi kuu Tanzania Bara, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini dar es Salaam, Stori kubwa kwenye mchezo huo ni Fiston Kalala Mayele ambaye amefunga mabao matatu, Hat trick baada ya kukaa muda mrefu bila kufakamia nyavu kwenye ligi kuu inayoendelea huku goli lingine likifungwa...
ULAYA NI ULAYA TU….WAFANYAKAZI REAL MADRID WAPEWA NDINGA MPYAA…GARI MOJA BIL 3…
Wachezaji na Wafanyakazi wote wa Real Madrid wamezawadiwa magari ya kifahari aina ya BMW. Kama ilivyoripotiwa na Jarida la Daily Mail limesema kwamba kila mchezaji atapokea gari aina ya BMW lenye thamani ya kiasi cha Tsh. Bilioni 3. Wachezaji na wafanyakazi wa Madrid wanaruhusiwa kuchagua gari kati ya matoleo ya iX na i4 na rangi yoyote watakayopenda. Real Madrid awali ilikua na...
KAZE : YANGA KUWA ‘UNBEATEN’ NI FAIDA….KUNA WATU WANATUOGOPA AFRIKA NZIMA..
Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Cedrick Kaze amesema Rekodi ya UNBEATEN haiwapi Presha wao kama wahusika, na badala yake imekua ikiwasaidia kuwapa matokeo katika Michezo inayowakabili. Young Africans inashikilia Rekodi ya kucheza bila kufungwa ‘UNBEATENA’ tangu msimu uliopita 2021/22, ikicheza michezo 45 ya Ligi Kuu Tanzania, leo Alhamis (Novemba 17) ikitarajia kukutana na Singida Big...
KISA KOCHA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA…WADAU WAMKALIA KOONI MANGUNGU…
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC Murtaza Mangungu amewataka wadau wa Soka nchini Kuheshimu na Kuamini ufafanuzi uliotolewa na Klabu hiyo kuhusu Kocha wa Makipa Muharami Said Mohammed maarufu ‘Shilton’. Simba SC ilitoa taarifa za kutomtambua Kocha huyo kama Mwajiriwa wake, baada ya kutoka kwa taarifa za kutuhumiwa na dawa za kulevya iliyotolewa jana Jumanne (Novemba 15), Kamishna Jenerali wa...
BAADA YA ‘KUIBANJUA KIMOKO’ NAMUNGO…MGUNDA AFUNGUKA YA MOYONI SIMBA..
Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC umempa nafasi Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Ramadhana Mgunda, kuwashukuru Wachezaji wake kwa kazi kubwa walioifanya jana Jumatano (Novemba 16), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam. Bao la ushindi la Simba SC lilipachikwa wavuni na Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Moses Phiri dakika 31, na kuifanya klabu hiyo kufikisha...
UKWELI MCHUNGU…SIMBA SC WASIPOJIANGALIA KATIKA HAYA…HATA HUKO KIMATAIFA WASAHAU…
Kuna ukweli ambao mashabiki wa Simba wengi hawataki kuusikia kwa kuwa wameaminishwa msimu huu wana kikosi bora sana. Lakini ukisimama karibu na uwanja ukachunguza vizuri ufanisi wa kikosi cha kwanza na halafu ukageuka nyuma kuangalia wanaopasha pale benchi kisha walioko jukwaani utagundua kuna sehemu kuna tatizo. Simba inahitaji wachezaji mbadala wenye uwezo wa kuipa matokeo bora. Yaani kikitoka kitu kiingie kitu....