M-BET WAFANYA KWELI KWA SIMBA QUEEN’S…WATOA MKATABA MNONO KUPITA YOTE…
Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-BET imeinga mkataba wa miaka mitano na klabu ya Simba Queens wenye thamani ya Sh bilioni 1. Simba Queens kwa sasa wapo mjini Rabat, Morocco ikishiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mkurugenzi wa masoko wa M-BET Tanzania Allen Mushi alisema kuwa wameamua kuingia mkataba na timu hiyo kutokana na mafanikio makubwa ya wa timu...
KUHUSU UBORA WA AZAM…MGUNDA KAKUNA KICHWA WEE..KISHA KWA UPOOLE AKASEMA HILI…
Kocha mkuu wa klabu ya Simba Juma Mgunda amesema wanakwenda kucheza mchezo wa kesho dhidi ya klabu ya Azam huku wakiwaheshimu klabu hiyo, Lakini watahitaji alama tatu katika mchezo huo. Mgunda amezungumza kua mchezo wa derby ulishamalizika hivo mchezo unaofuata ni dhidi ya Azam, Na walijua baada ya kumaliza mchezo wa derby mchezo ambao ungefata ni dhidi ya wanalambalamba na...
KUELEKEA MECHI YA KESHO …MASTAA HAWA WANNE WA SIMBA KUIKOSA AZAM FC…
Nyota wanne wa Simba wataukosa mchezo wa ligi kesho dhidi ya Azam kutokana na majeraha waliyonayo pamoja na kadi za njano. Mchezo huo wa ligi utapigwa kesho alhamisi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo Azam wakiwa na pointi 11 huku Simba wakiwa nazo 14. Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema “Tunamshukuru Mungu maandalizi yamekamilika mpaka hivi sasa...
KOCHA AZAM FC AITEMEA CHECHE SIMBA SC….APANIA KUMTIBULIA JAMBO MGUNDA…
Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC Kalimangonga Ramadhan Mtoro Ongala, amefunguka kwa mara ya kwanza tangu alipokabidhiwa jukumu la kukiongoza kikosi cha ‘Wababe wa Chamazi’. Kali aliyewahi kucheza Azam FC na Young Africans alikabidhiwa jukumu hilo kwa kusaidiwa na Mchezaji Mkongwe Agrey Morris, baada ya kutimuliwa kwa Kocha kutoka nchini Ufaransa Denis Lavagne. Ongala amesema ana uhakika timu itafanya vizuri katika...
KUHUSU ISHU YA KUFUKUZWA YANGA…NABI AVUNJA UKIMYA..ADAI YUKO TAYARI HATA SASA ‘KUSEPA…’
Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Mohamed Nabi, amekiri kushangazwa na taarifa za kutimuliwa kwenye klabu hiyo, ili hali bado anaendelea na majukumu yake. Jana Jumanne (Oktoba 25) Gazeti la Mwanaspoti liliibuka na taarifa za kutimuliwa kwa kocha huyo kutoka nchini Tunisia, huku likimtaja Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Uganda Vipers SC Roberto Oliveira Gonçalves...
PAMOJA NA ‘KUSHAINI’…PHIRI AFUNGUKA MTU ANAYETAKA KUCHEZA NAYE PAMOJA SIMBA…
Mshambuliaji kutoka nchini Zambia na Klabu ya Simba SC Moses Phiri amesema mafanikio yake msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, yatategemea sana ushirikiano mkubwa atakaoupata kutoka kwa Kiungo Clatous Chotta Chama. Phiri ambaye hadi sasa ndio kinara wa upachikaji mabao kwenye kikosi cha Simba SC, amekuwa gumzo midomoni mwa Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo ya Msimbazi, kutokana na...
BAADA YA ‘KUMTESA’ MANULA JUZI…AZIZ KI AIBUKA NA HILI JIPYA…AFUNGUKA KUHUSU MAHABA YAKE…
AZIZ Ki kiungo mshamuiaji wa Yanga amesema kuwa anapenda kufunga ama kutengeneza nafasi za mabao akiwa ndani ya uwanja. Nyota huyo ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo alijiunga na kikosi hicho akitokea ASEC Mimosas. Oktoba 23,2022 alifunga bao la pili ndani ya ligi ambapo alimtungua Aishi Manula kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18. Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya...
MZAMIRU AANIKA SIRI ZAKE SIMBA…AFUNGUKA ISHU YA MKUDE KUPIGWA BENCHI HUKU YEYE AKIANZA…
Kiungo mkabaji wa Simba, Mzamiru Yassin amefunguka siri ya ubora alionao sasa ndani ya timu yake kuwa ni kurudia kutazama mechi alizocheza ili kutambua makosa yake asiyarudie mechi inayofuata. Mzamiru amekuwa chaguo la kwanza chini ya Kaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda tangu amepewa timu hiyo akichukua nafasi ya Zoran Maki aliyetimkia Misri. Mzamiru alisema hajabahatisha kuingia kikosini moja kwa...
M-BET WAMWAGA MAMILIONI SIMBA QUEEN’S….BARBARA AFUNGUKA ‘WALIVYOVUTANA…’
Klabu ya Simba Queens imelamba dili la udhamini kutoka kwa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet lenye thamani ya shilingi Bilioni 1. Simba Queens walelamba rasmi dili hilo leo Oktoba 26, 2022 ambapo CEO wa klabu, Barbara ameweka wazi kuwa, mkataba huo ni wa kwanza kwa upande wa timu za wanawake. “Tulivutana kwa muda mrefu na M Bet mapaka kufikia...
GSM AZUIA NABI KUFUKUZWA…VIGOGO WATAFUTANA…MGUNDA AILIA ‘TAIMINGI’ AZAM FC…
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la MwanaSpoti la leo Jumatano.