WAKATI WAKISHINDA WANAKUTANA WA WAMISRI…MPOLE KUWAPA NGUVU GEITA GOLD LEO…WAKIZEMBEA NDIO BASI TENA…
MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, George Mpole ameanza rasmi mazoezi na kikosi hicho kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Hilal Alsahil ya Sudan, mchezo utakaopigwa leo katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.Nyota huyo alikosa mechi ya kwanza iliyopigwa Sudan Septemba 11 kutokana na kusumbuliwa na Malaria huku akishuhudia kikosi hicho...
AMEANZAA …..MORRISON AZUA HOFU YANGA…NABI AJILAUMU KUMUAMINI NA KUMPA NAFASI….DAKTARI YANGA AFUNGUKA…
YANGA inarudi uwanjani leo kumalizana na Zalan ya Sudan Kusini katika mchezo wa marudiano utakaopigwa saa 1:00 usiku katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini staa mmoja tu muhimu, Bernard Morrison ‘BM33’ amezusha hofu kubwa kwa benchi la ufundi la timu hiyo.Tangu Morrison acheze mechi ya mwisho dhidi ya Azam iliyoisha kwa sare ya...
HIVI NDIVYO YANGA YA INJINIA HERSI INAVYONUKA PESA AISEE…BILIONI 9.1 ZATENGWA KWA UJENZI WA UWANJA…
Ukisema fedha inaongea, hutakosea kwani mabosi wa Yanga wameamua kuweka mikakati mizito kuhakikisha nyota wa kikosi hicho wanaishi kishua kwa kuboresha mishahara ya wachezaji, lengo likiwa ni vijana hao kutimiza majukumu yao ya uwanjani kuanzia michuano ya Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.Hiyo ikiwa ni siku chache tangu uongozi wa timu hiyo uingie mkataba wa miaka mitano...
BAADA YA KELELE ZA TIMU FULANI FULANI KUHONGA ILI ZISHINDE…TAKUKURU WAIBUKA NA KAULI HII ….
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imefanya kikao kazi na wadau mbalimbali, kilichojadili matokeo uchambuzi wa mfumo wa usimamizi wa fedha za maendeleo ya mpira wa miguu kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa lengo la kuweka mikakati ya kudhibiti mianya ya rushwa inayoweza kujitokeza katika eneo hilo.Kikao kazi hicho kimefanyika Septemba 15, 2022 jijini Dodoma,...
HILI HAPA KINDA LA YANGA LINALOWATOA UDENDA WAFARANSA…MARSEILLE WATUMA MTU KUMBEBA…ZAHERA ATEMA ‘UBUYU’…
Klabu ya Yanga imepokea mualiko wa mshambuliaji wake kinda, Clement Mzize ambaye anatakiwa na klabu kubwa ya Olympic Marseille ya Ufaransa.Mkurugenzi wa ufundi wa Yanga Mwinyi Zahera amesema tayari Marseille wameshatuma mualiko wa kinda huyo kutakiwa kwa majaribio ya wiki mbili yatakayofanyika nchini humo.Marseille ambao wamemuona kinda huyo katika Mashindano ya soka la vijana chini ya miaka 20 ambapo...
AHMED ALLY : DEJAN NAYE HAKUWA CHAGUA LA KOCHA MAKI…SABABU YA KWANINI HACHEZI HIZI HAPA…
Semaji la Simba SC, Ahmed Ally amesema Mzungu wa Simba Dejan bado yupo sana kwenye kikosi chao hivyo wale wanaodhani ataondoke, wakae kwa kutulia.Ahmed ameyasema hayo mapema jana Septemba 16, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV ambapo alipoulizwa kuhusu suala la Dejan kama alikuwa chaguo la aliyekuwa Kocha Mkuu Zoran Maki na ameeondoka hivyo huwenda naye akaondoka ndipo...
MAMBO YAMEKUWA MAMBO SIMBA….MGUNDA APIGIWA KAMPENI YA UKOCHA…MASHABIKI HAWAELEWI NENO JUU YAKE…
Anatosha! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mashabiki, wapenzi na baadhi ya mastaa wa zamani wa kikosi cha Simba kuridhishwa na ubora wa Kocha Juma Mgunda.Mgunda aliyekuwa kocha wa Coastal Union, aliteuliwa na Simba Septemba 7, kocha mkuu wa muda wa timu hiyo akirithi mikoba ya Zoran Maki aliyeondoka kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.Kwa muda mfupi akiwa Simba, Mgunda...
WAKATI SIMBA NA YANGA WAKIWA NA UHAKIKA CAF…GEITA GOLD WAAPA KUWEKA REKODI YAO KIMATAIFA LEO…
Kocha Msaidizi wa Geita Gold, Mathius Wandiba amesema hawatarajii kurudia makosa waliyoyafanya mechi iliyopita wanahitaji ushindi ili waweze kusonga hatua inayofuata.Geita Gold wanatarajia kuwa wenyeji wa Hilal Alhasil ya Sudan leo mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 ugenini.Akizungumza na waandishi wa habari, Wandiba alisema wamefanyia...
SAA KADHAA KABLA YA KUSHUKA DIMBANI LEO….YANGA WAPEWA ‘USHINDI WA MEZANI’ DHIDI YA WASUDANI…ISHU NZIMA IKO HIVI…
Beki wa zamani wa Yanga, Muarami Issa 'Marcelo' ameukubali mziki wa timu hiyo huku akiipa nafasi ya kushinda katika mchezo wa leo dhidi ya Zalan ya Sudan Kusini na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa msimu huu.Yanga itaikaribisha Zalan ya Sudan Kusini leo Jumamosi saa 1 usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwa mchezo wa...
MBALI NA KUPIGWA JUZI…MWAKINYO AZIDI KUTAKATA DUNIANI….ISHU NZIMA IKO HIVI…
Licha ya kupigwa kwa Technical Knock Out (TKO), Hassan Mwakinyo amepanda kwa nafasi mbili katika viwango vya ubora wa ngumi za kulipwa vya dunia.Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi wa dunia (Boxrec), Mwakinyo sasa ni bondia wa 38 kati ya 1,953 duniani kwenye uzani wa super welter akipanda kwa nafasi mbili kutoka ya 40 aliyokuwa awali kabla ya pambano...