Tuesday, January 13, 2026
Home Blog Page 2955

Stand United yashuka rasmi daraja!

0

Timu ambayo ilikuwa inasubiriwa kushuka daraja kuungana na African Lyon imepatikana rasmi. Stand United ya Shinyanga rasmi wameshuka daraja baada ya kufungwa na JKT Tanzania kwa goli 2-0 na JKT Tanzania.

Timu mbili ambazo zitacheza playoff (Michezo ya mitoano ) ni Kagera Sugar aliyeshika nafasi ya 18 na Mwadui FC aliyeshika nafasi ya 17.

Mwadui na Kagera watacheza na Pamba FC ya Mwanza na Geita Sports ya Geita. Mshindi wa playoff atapanda ligi kuu Tanzania bara msimu ujao tena

# Timu P W D L GD Pts
1 Simba SCSimba SC 38 29 6 3 62 93
2 Yanga SC 38 27 5 6 29 86
3 Azam FC 38 21 12 5 33 75
4 KMC FC 38 13 16 9 15 55
5 Mtibwa Sugar FC 38 14 8 16 1 50
6 Lipuli FC 38 12 13 13 -8 49
7 Mbeya City FC 38 13 9 16 -1 48
8 Coastal Union FC 38 11 15 12 -10 48
9 Ndanda FC 38 12 12 14 -12 48
10 JKT Tanzania SC 38 11 14 13 -6 47

The post Stand United yashuka rasmi daraja! appeared first on Kandanda.

RUVU YAKOMAA KUBAKI TP, MATOKEO NA TIMU ZILIZOSHUKA DARAJA HAYA HAPA

0

LEO Ligi Kuu Bara Tanzania ilikuwa inafika tamati ambapo mbivu na mbichi zimejulikana kuanzia bongwa na zile zitakazoshuka daraja.

Bingwa ni Simba ambaye amemaliza ligi akiwa na jumla ya pointi 93.

African Lyon na Stand United zimeshuka daraja moja kwa moja.

Kagera Sugar ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 44 ikiwa na tofauti ya mabao ya kufungwa ambapo Stand United wamefungwa jumla ya mabao 50 na Kagera Sugar imefungwa jumla ya mabao 43.

Matokeo ya leo kiujumla ni haya hapa:

FT: Coastal Union 0-0 Singida United.

FT: Mbeya City 0-0 Biashara United.

FT: Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC.

FT: Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC (Fully Zullu Maganga 25’ p) . .
.

FT: JKT Tanzania 2-0 Stand United (Samweli Kamuntu 51’, Najimu Maguli 73’).
.
.
FT: Ndanda SC 1-3 Mwadui FC (Kigi Makasi : Ottu Joseph 39’, 41’, Salim Aiyee 61’) .
.
.
FT: Yanga SC 0-2 Azam FC (Daniel Amoah 45’+2, Mudathir Yahya 50’).
.
.
FT: Mbao FC 1-1 Kagera Sugar (Hebert Lukindo 60’ : Ally Ramadhan 20’).
.
.
FT: Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC (Benjamini Asukile 29’, Adam Adam 48’, 85’ : Seif Rashid 46’).
.
.
FT: African Lyon 0-2 KMC FC (Cliff Buyoya 21’, 17’)
.

NABY KEITA WA LIVERPOOL KUIKOSA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA DHIDI YA SPURS

0


Naby Keita wa Liverpool ataukosa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Tottenham kutokana na majeruhi.

Keita alipata majeruhi hayo kwenye mchezo wa  nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona.

Kiungo huyo huyo amesafiri na timu kwenye kambi ya Marbella na wachezaji wenzake kwenye maandalizi ya awali ya mchezo wa fainali.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amethibitiha kwamba hatamtumia mshambuliaji huyo kwenye mchezo wake wa fainali utakaopigwa Juni Mosi.


TPL: YANGA 0-0 AZAM FC

0

MCHEZO wa sasa unaoendelea uwanja wa Taifa kati ya Yanga na Azam FC ni kipindi cha kwanza na hakuna ambaye ameliona lango la mpinzani wake.

Mchezo huu una ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ambazo zinatafuta heshima kwenye uwanja wa Taifa leo ikiwa ni mchezo wa mwisho kwa msimu huu.

KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHOANZA DHIDI YA YANGA

0
Kikosi rasmi cha Azam FC kitakachoanza leo dhidi ya Yanga


Kikosi kitakachoanza
16 Razak Abalora
57 Lusajo Mwaikenda
03 Daniel Amoah
05 Yakubu Mohammed
06 Agrey Moris (c)
22 Salmin Hoza
27 Mudathir Yahya
08 Salum Abubakar
07 Obrey Chirwa
11 Donald Ngoma
26 Bruce Kangwa

Akiba


Mwadini

 Mwasapili
 Mwantika
 Domayo
Peter
 Lyanga
 Singano.

Mechi nne kufa na kupona Leo!

0

Mpaka sasa hivi African Lyon ndiyo timu pekee ambayo hatutokuwa nayo kwenye ligi kuu msimu ujao.

Kwa utaratibu uliopo, timu zinazoshika nafasi ya 19 na 20 zitashuka moja kwa moja daraja na kwenda ligi daraja la kwanza.

Timu mbili zitakazoshika nafasi ya 17 na 18 zitacheza Play Off dhidi ya timu ambazo zimeshiriki ligi daraja la kwanza , ambapo mpaka sasa hivi ni Pamba na Geita Sports ambazo zitacheza Play Off.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi kuu msimu huu, anayeshika nafasi ya 11 kushuka chini anaweza kushuka daraja msimu huu.

Timu inayoshika nafasi ya 11 ni Singida United yenye alama 11 na timu inayoshika nafasi ya 19 ni Mwadui FC yenye alama 41.

Zifuatazo ni mechi ambazo zinaweza kutoa maamuzi ya timu ambazo zitashuka daraja msimu huu.

1. JKT vs Stand United
2. Mbao FC vs Kagera Sugar
3. Mwadui FCvs Ndanda
4. Ruvu Shooting vs Alliance Schools FC

RUVU SHOOTING

Mpaka sasa hivi inashika nafasi ya 18 na ina alama 42, kitu pekee ambacho kitaisaidia Ruvu Shooting ni kushinda ili iweze kufikisha alama 45 ambazo zitaishusha Singida United katika nafasi yake ya 11 kama Singida United atafungwa.

MWADUI

Ndiyo timu ambayo inatazamiwa kushuka daraja msimu huu, inashika nafasi ya 19 na ina alama 41 mpaka sasa. Kama itashinda itapata jumla ya alama 44 ambazo zitampeleka katika nafasi ya 12 kama Biashara United itafungwa ambayo na yenyewe ina alama 44.

JKT TANZANIA

Salama pekee ya JKT Tanzania ni wao kupata sare au kushinda, kitu hiki kitawafanya wawe mbali na shimo la kushuka daraja msimu huu.

KAGERA SUGAR

Ina alama 43 mpaka sasa hivi ikiwa na katika nafasi ya 17, matokeo pekee ni yeye kushinda na timu zingine anazoshindana naye zifungwe na akishinda atapata alama 46 ambazo zitamsaidia sana.

STAND UNITED
Inashika nafasi ya 14 ikiwa na alama 44 kitu pekee inachohitaji ni alama moja au ushindi huku akiziombea timu zingine pinzani zipoteze michezo yao.

MBAO
Timu nyingine inayohitaji alama moja au alama tatu huku ikiombea timu zingine zifungwe ni hii.

The post Mechi nne kufa na kupona Leo! appeared first on Kandanda.

329,001FansLike
12,344FollowersFollow
16,900SubscribersSubscribe

EDITOR PICKS