Home Uncategorized BREAKING NEWS: BODI YA LIGI YAKIRI KUBORONGA, YAISHUSHA STAND UNITED, KAGERA YAENDA...

BREAKING NEWS: BODI YA LIGI YAKIRI KUBORONGA, YAISHUSHA STAND UNITED, KAGERA YAENDA PLAY OFF


Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imetangaza kufanya marekebisho katika msimamo wa Ligi Kuu Bara huku ikisema itachukua hatua kwa watunza takwimu wake waliopotosha.

Awali ilionekana Kagera Sugar ndio imeteremka lakini Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema marekebisho waliyofanya Stand United inashuka na nafasi ya juu inakwenda kwa Kagera Sugar.

Maaana yake Stand United ndio iliyoteremka daraja na nafasi ya kucheza Play Off inakwenda kwa Kagera Sugar.

Kagera Sugar itaivaa Pamba Juni 2 katika mechi ya Play Off na mshindi atacheza Ligi Kuu Bara na Mwadui FC itamenyana na Geita.

Baada ya ligi kumalizika jana, kumekuwa na gumzo na kizumgumkuti huku watu wakiwa hawajui timu iliyoteremka kwa kuwa tawimu za Gazeti la Championi na Azam Tv zilionyesha aliyeshuka ni Stand United huku takwimu za bodi ya ligi zilionyesha ni Kagera Sugar ndio iliyoteremka.

SOMA NA HII  SIMBA WAOGA MINOTI KUTOKA CAF ISHU IKO HIVI