Home Uncategorized Mechi nne kufa na kupona Leo!

Mechi nne kufa na kupona Leo!

Mpaka sasa hivi African Lyon ndiyo timu pekee ambayo hatutokuwa nayo kwenye ligi kuu msimu ujao.

Kwa utaratibu uliopo, timu zinazoshika nafasi ya 19 na 20 zitashuka moja kwa moja daraja na kwenda ligi daraja la kwanza.

Timu mbili zitakazoshika nafasi ya 17 na 18 zitacheza Play Off dhidi ya timu ambazo zimeshiriki ligi daraja la kwanza , ambapo mpaka sasa hivi ni Pamba na Geita Sports ambazo zitacheza Play Off.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi kuu msimu huu, anayeshika nafasi ya 11 kushuka chini anaweza kushuka daraja msimu huu.

Timu inayoshika nafasi ya 11 ni Singida United yenye alama 11 na timu inayoshika nafasi ya 19 ni Mwadui FC yenye alama 41.

Zifuatazo ni mechi ambazo zinaweza kutoa maamuzi ya timu ambazo zitashuka daraja msimu huu.

1. JKT vs Stand United
2. Mbao FC vs Kagera Sugar
3. Mwadui FCvs Ndanda
4. Ruvu Shooting vs Alliance Schools FC

RUVU SHOOTING

Mpaka sasa hivi inashika nafasi ya 18 na ina alama 42, kitu pekee ambacho kitaisaidia Ruvu Shooting ni kushinda ili iweze kufikisha alama 45 ambazo zitaishusha Singida United katika nafasi yake ya 11 kama Singida United atafungwa.

MWADUI

Ndiyo timu ambayo inatazamiwa kushuka daraja msimu huu, inashika nafasi ya 19 na ina alama 41 mpaka sasa. Kama itashinda itapata jumla ya alama 44 ambazo zitampeleka katika nafasi ya 12 kama Biashara United itafungwa ambayo na yenyewe ina alama 44.

JKT TANZANIA

Salama pekee ya JKT Tanzania ni wao kupata sare au kushinda, kitu hiki kitawafanya wawe mbali na shimo la kushuka daraja msimu huu.

KAGERA SUGAR

Ina alama 43 mpaka sasa hivi ikiwa na katika nafasi ya 17, matokeo pekee ni yeye kushinda na timu zingine anazoshindana naye zifungwe na akishinda atapata alama 46 ambazo zitamsaidia sana.

STAND UNITED
Inashika nafasi ya 14 ikiwa na alama 44 kitu pekee inachohitaji ni alama moja au ushindi huku akiziombea timu zingine pinzani zipoteze michezo yao.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII

MBAO
Timu nyingine inayohitaji alama moja au alama tatu huku ikiombea timu zingine zifungwe ni hii.

The post Mechi nne kufa na kupona Leo! appeared first on Kandanda.