Home Uncategorized HIZI NDIZO TIMU ALIZOKIPIGA NYOTA MWENYE RASTA ANAYEWINDWA NA YANGA

HIZI NDIZO TIMU ALIZOKIPIGA NYOTA MWENYE RASTA ANAYEWINDWA NA YANGA


YASSIN Salum beki wa Polisi Tanzania anayekipiga ndani ya Polisi Tanzania mwenye rasta kichwani mabosi wa Yanga inaelezwa kuwa wamemuweka kwenye hesabu ili kuipata saini yake.

Nyota huyo kabla ya kuibukia Polisi Tanzania aliwahi kucheza ndani ya Stand United ambayo kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza hiyo ilikuwa ni mwaka 2014.

Aliibukia ndani ya Polisi Tanzania iliyo chini ya Malale Hamsini akitokea Klabu ya Polisi Dodoma.

 Akiwa Stand United, alicheza msimu mmoja na 2015/16 akacheza Coastal Union, 2016/17 na 2017/18 alicheza Mwadui, 2018/19 akacheza Ndanda.

SOMA NA HII  KILICHOIPOTEZA YANGA UWANJA WA UHURU MBELE YA KMC HIKI HAPA