Home Uncategorized SIMBA WAPOKELEWA LEO DAR NA MASHABIKI KIBAO, BODABODA ZATIA FORA

SIMBA WAPOKELEWA LEO DAR NA MASHABIKI KIBAO, BODABODA ZATIA FORA


MASHABIKI wa Simba leo wameungana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi kuipokea timu kutoka Morogoro ikiwa imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Mashabiki hao leo walikuwa wamejitokeza wakiwa na bodaboda zao na kuwafanya baaadhi ya wachezaji akiwemo mlinda mlango namba mbili, Deogratius Munid ‘Dida’ kuonesha uwezo wake wa kukanyaga mafuta.

Mabingwa hao wa TPL msafara wao umeanzia Morogoro na walipofika Kibaha Stand wachezaji walipanda kwenye gari la wazi wakiwa na kombe lao wakiwaonyesha mashabiki ambao walijitokeza barabarani.

Msafara wa mashabiki uliacha shughuli kwa muda na kuungana na mabingwa hao, msafara ulipita bararabara ya Morogoro maeneo ya Kibabamba, Kimara, Mbezi, Ubungo mpaka Manzese pia.

Maeneo ya Msimbazi yalipo makao makuu ya Simba, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikabidhiwa kombe na nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kabla ya msafara kuunganisha safari kupitia Magomeni na kuishia maeneo ya Sea Escape ilipo kambi ya wachezaji.
SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: AZAM FC WALIKUWA WANAKUTANA NA TIMU NDOGO