Home Uncategorized KOCHA MKUU WA BARCELONA AKALIA KUTI KAVU

KOCHA MKUU WA BARCELONA AKALIA KUTI KAVU

KUNA dalili za kibarua cha kocha Ernesto Valverde `kuota nyasi’ kufuatia kitendo cha Barcelona kuamua kuwasiliana na Roberto Martinez.

Gazeti la Sport limedai kuwa viongozi wa Barcelona wamezungumza na Martinez, ambaye kwa sasa anainoa timu ya taifa yaUbelgiji.

Viongozi wa Barcelona inasemekana wanataka kuachana na Valverde baada ya kuchukizwa na matokeo ya karibuni ya timu hiyo.Pamoja na kutwaa ubingwa wa La Liga, lakini
Barcelona ilitolewa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Liverpool.

Barcelona ilishinda mchezo wa kwanza mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Nou Camp lakini ilibweteka na kupigwa mabao 4-0 ugenini kwenye mchezo wa marudiano licha ya Liverpool bila kuwa na mastraika wake tegemeo, Mohamed Salah na Roberto Firmino.

Pia majuzi imelizwa katika fainali ya Copa delRey baada ya kulala kwa Valencia mabao 2-1.Uongozi wa Barcelona umepanga kumtimua Valverde na wanataka Martinez achukue nafasi hiyo haraka.

Makocha wengine wanaotakiwa na Barcelonani pamoja na Unai Emery wa Arsenal na Max Allegri, ambaye aliachana na Juventus hivi karibuni.

SOMA NA HII  AHAMED ALLY AWEKA WAZI KILICHOMPELEKA GAMONDI KWENYE MECHI YA SIMBA JANA