Home Uncategorized MBADALA WA ROMELU LUKAKU UNITED NI HUYU HAPA

MBADALA WA ROMELU LUKAKU UNITED NI HUYU HAPA


MANCHESTER United wanampigia hesabu za kumsajili mshambuliaji wa kikosi cha Frankfurt, Sebastien Haller kwa ajili ya msimu ujao.

United wanaitaka saini ya mchezaji huyo ili awe mbadala wa nyota wao Romelu Lukaku ambaye anahitaji kusepa ndani ya kikosi hicho.

Kikosi cha Inter Milan kimeonyesha nia ya kupata saini ya mchezaji huyo ambaye ni mshambuliaji anayekipiga timu ya Taifa pia ya Ubelgiji.

Mabosi wa United wapo tayari kumuuza Lukaku kwa dau la Euro milioni 80 kwa kuwa wanajua kwamba Lukaku ni chaguo la Antonie Conte ambaye inasemekana atakuwa meneja wa kikosi hicho.

Wafuatiliaji wa wachezaji kutoka United wamesema kuwa Haller atakuwa ni mbadala wa Lukaku kutokana na uwezo wake wa kutupia mabao ambapo kwenye ligi ya Bundesliga amefunga jumla ya mabao 15 kwenye mechi zake 23 za mwanzo.

SOMA NA HII  PACHA HIZI NDANI YA MSIMU MPYA WA 2020/21 ZINAPEWA NAFASI YA KUBAMBA