Home Uncategorized GARI LA BIA LAIBIWA

GARI LA BIA LAIBIWA

MAMTONI kweli kuna mambo tena si madogo! Kampuni moja ya bia ijulikanayo kama Unknown Brewery imeibiwa gari lake la bia na kutoa ofa ya bia za bure kwa atakayelirudisha.


Kwa kutumia kamera maalum za CCTV, kampuni hiyo ilipoteza gari lake ambalo lilikuwa limebeba bia na baada ya kupita dakika 42 waliliona kwenye kamera likiwa limeshikiliwa na vijana watatu eneo la Charlotte, North Carolina.

Baada ya kuliona waliweka tangazo kwenye ukurasa wao wa Instagram kwa kuandika: “Popote utakapoliona gari hili kampuni itakuzawadia bia za bure na hata kama ni wewe umeliona bado kampuni itakupa bia za bure. Wasiliana nasi kwa meseji (Direct Massage ‘DM’).”

Ndani ya saa moja tayari meseji nyingi zilijaa zikitaka kupatiwa ofa ya bia kwanza kisha kulifikisha gari mahali husika

SOMA NA HII  MENEJA WA MANCHESTER CITY AWEKA REKODI YA AINA YAKE