Home Uncategorized AISHI MANULA APIGWA PINI RASMI MIAKA MITATU

AISHI MANULA APIGWA PINI RASMI MIAKA MITATU

MLINDA mlango wa Simba, Aishi Manula ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Kariakoo, Msimbazi.


Manula anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa rasmi kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo baada ya jana mchezaji John Bocco kutangazwa rasmi kwamba ameshamalizana na klabu hiyo kwa kuongeza mkataba wa maika miwili.


Kwa sasa Manula yupo nchini Misri akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambayo imeweka kambi kwa ajili ya michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21.
SOMA NA HII  VIDEO:UCHAMBUZI KUHUSU YANGA KUINGIA MAKUBALIANO NA LA LIGA