Home Uncategorized BEKI MATATA KUTUA MAN UNITED

BEKI MATATA KUTUA MAN UNITED


MAN United inasemekana ipo kwenye hatua za mwisho za kumsajili beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-bissaka, ambaye wamekuwa wanamfukuzia wa muda mrefu.

Muda mwingi wa msimu wa 2018, Manchester United imekuwa inatajwa kumwania WanBissaka, ambaye anang’ara kama beki wa pembeni.

Wan-Bissaka anahesabiwa kama miongoni mwa mabeki bora wa kulia kwenye Ligi Kuu England. Manchester United inasemekana imekubali kulipa ada ya pauni milioni 60 (Sh. bilioni 174) ili kumchukua WanBissaka, ambaye pia anachezea timu ya vijana ya England wenye umri wa chini ya miaka 21.

Dili baina ya Manchester United na Wan-Bissaka linatazamiwa kukamilika katika siku chache zijazo. Beki mwenyewe naye inaaminika anataka sana kujiunga na Manchester United.

Wan-Bissaka aling’ara na Crystal Palace katika msimu wa 2018/19 ambapo alicheza jumla ya mechi 39 katika mashindano yote. Manchester United ina tatizo la beki wa kulia, ambapo kwa kiasi kikubwa imekuwa inamtegemea beki mkongwe Ashley Young. Wan-Bissaka akitua Manchester United atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na timu hiyo baada ya winga Daniel James.

SOMA NA HII  YANGA YAANZA KUIVUTIA KASI SIMBA MDOGOMDOGO