Home Uncategorized KIKOSI CHA YANGA CHATUA SALAMA ZANZIBAR, LAMINE ‘OUT’

KIKOSI CHA YANGA CHATUA SALAMA ZANZIBAR, LAMINE ‘OUT’

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze leo Januari 4 kimetia timu kwenye ardhi ya Visiwa vya Zanzibar. 


Timu hiyo itaanza kibarua cha kusaka taji hilo la heshima lililo mikononi mwa Mtibwa Sugar ambao walitwaa taji hilo kwa kuifunga bao 1-0 Simba msimu wa 2020.


Miongoni mwa nyota ambao imeongozana nao ni pamoja na kipa namba moja Metacha Mnata, Farouk Shikalo, Wazir Junior, Michael Sarpong, Zawd Mauya,Paul Godfrey, Carlos Carlinhos.


Mchezo wao wa kwanza ni kesho Januari 5 ambapo watatupa kete yao ya Kwanza mbele ya Jamhuri ya Visiwani Zanzibar. 


Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Amaan, majira ya saa 8:15 usiku.Beki Lamine Moro atakosekana kwa kuwa yupo zake Ghana ambapo amekwenda mwa ajili ya mapumziko mafupi. 

SOMA NA HII  MASHINE HII YA KAZI YATAJWA KUTUA LEO KUMALIZANA NA YANGA