Home Uncategorized MTIBWA SUGAR: TUPO TAYARI KUREJEA KWENYE USHINDANI

MTIBWA SUGAR: TUPO TAYARI KUREJEA KWENYE USHINDANI


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Mtibwa Sugar tayari wameshaanza mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa dhidi ya mechi za ligi ambazo zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 13.

 Masuala ya michezo yalisimamishwa na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona, Machi 17 ila kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya ligi kwa kueleza kuwa maambukizi yamepungua.

“Kwa namna yoyote ile wachezaji wangu wapo tayari kurejea kwenye ushindani kutokana na wachezaji kuwa tayari kufanya kazi yao.

“Wakati wa mapumziko wachezaji walikuwa wanaendelea na program nyumbani hivyo hapa wanakuja kuendelea pale ambapo waliishia kwani kikubwa kwa mchezaji ni kuendelea kufanya mazoezi muda wote bila kuchoka,” amesema.

Juni 20, Mtibwa Sugar itamenyana na Coastl Union Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YASHINDA MBELE YA CHIPUKIZI