Home Uncategorized AJIBU PASUA KICHWA, AWAZIMIA SIMU MABOSI WA TP MAZEMBE

AJIBU PASUA KICHWA, AWAZIMIA SIMU MABOSI WA TP MAZEMBE


UNAAMBIAWA TP Mazembe, bado wamemkomalia nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu ambaye usajili wake uliingia doa kwa kushindwana kwenye malipo.

Wakala wa TP Mazembe, Patrick Mazembe amesema kuwa bado Mazembe wanahitaji huduma ya mchezaji huyo ambaye msimu wa 2018/19 alikuwa ni kinara wa pasi za mwisho TPL baada ya kutoa jumla ya pasi 17.

“Mwanzo Ajibu alitusumbua kwa kutaka dau kubwa, kwa sasa tumeamua kumfuata Bongo, ila ametuzimia simu hivyo jitihada za kumtafuta zinaendelea kama tutaelewana naye basi atatua Mazembe,” amesema.


Imeelezwa kuwa Ajibu amesaini mkataba wa awali ndani ya Simba kwa muda wa miaka miwili.

SOMA NA HII  MASHAKA YA KOCHA MKUU LIGI KUU BARA NI KUSHUKA KWA VIWANGO VYA WACHEZAJI