Klabu ya Yanga inatarajia kufanya jambo kubwa ambalo litakalo wasogeza mbele kisoka na kuleta mapinduzi nchini, huku wakisema wao wamefanikiwa kwa asilimia kidogo katika kukusanya kiasi ambacho wao walikuwa wana malengo nacho cha kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 1.5
Fedha hizo zinatarajiwa kuwasilishwa siku ya kesho Jumamosi katika ukumbi wa Daimondi Jubilee kwa uongozi mpya wa klabu hiyo ilii kuangalia nini wanatakiwa kukufanya huku zingine zikiwa zinatarajiwa kugawiwa kwa kocha mkuu Mwinyi Zahera raiya wa Kongo ambaye ndiyo kocha anakinowa kikosi hicho kwa hivi sasa.