Home Uncategorized KUMEKUCHA NAMUNGO, WAGOMEA WACHEZAJI WA MAJARIBIO

KUMEKUCHA NAMUNGO, WAGOMEA WACHEZAJI WA MAJARIBIO


UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa kwa sasa haufikirii kusajili wachezaji wa majaribio na badala yake wanafanya kazi kubwa kusajili wachezaji wenye uwezo wa kushindana.

Akizungumza na Salehe Jembe, Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia amesema kuwa baada ya kikosi kupanda ligi kuu, hesabu kubwa ni kusuka kikosi cha ushindani na sio cha majaribio.

“unajua kwamba ushindani wa kwenye ligi ni tofauti na kule tulikokuwa sasa ili tufanye vizuri lazima tusajili wachezaji wenye uzoefu na ushindani na ndio maana kwa sasa tumeanza na wale waliopandisha timu Daraja kisha wenye uzoefu wanafuata,” amesema Namlia.

Mchezaji mmoja tu mpaka sasa ndiye wametangaza kumsajili kutoka timu nyingine ambaye ni Bigirimana Blaise kwa kumpa kandarasi ya mwaka mmoja akitokea Alliance.

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING WAMPAPASA BOSI WAO WA ZAMANI, CHUMA APELEKWA HOSPITALI