Home Uncategorized OKWI AGOMEA MKATABA SIMBA

OKWI AGOMEA MKATABA SIMBA


EMMANUEL Okwi amezidi kuwatia kiwewe Simba kwanza kutokana na kiwango anachokionyesha kwenye michuano ya Kombe la Afrika ‘Afcon’ kule Misri pili ni kuwa anazingua kusaini mkataba wa miaka miwili Msimbazi.

Okwi, raia wa Uganda, amefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mechi kwenye Afcon katika mchezo wa kwanza dhidi ya DR Congo ambapo yeye alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata.

Mechi iliyofuata, Okwi alifunga tena bao ambapo safari hii ilikuwa dhidi ya Zimbabwe na kuzidi kupandisha thamani yake kisoka.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa, mabosi wa Simba juzi walisafiri hadi Misri kwenda kumlainisha asaini mkataba wa miaka miwili ili aendelee kubaki Msimbazi.

Hata hivyo, Okwi ambaye ni kipenzi cha Wanasimba aligoma kusaini miaka miwili akitaka apewe mwaka mmoja hali ambayo iliwashtua mabosi hao jambo ambalo lilisababisha mvutano kiasi.

“Kutokana na hali hiyo kumekuwa na mvutano mkubwa lakini uongozi unapambana kuhakikisha unamshawishi ili aweze kukubali kusaini mkataba wa miaka miwili badala ya mmoja.

“Hatujajua ni kwa nini anataka apewe mwaka mmoja ila ngoja tusubiri tuone kwa sasabu kuna baadhi ya viongozi wetu wapo nchini Misri wakilishugulikia jambo hilo,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Kwa upande wake Okwi ambaye alihojiwa na kituo kimoja cha habari nchini, alikaririwa akisema kuwa kwa sasa ni ngumu kuzungumzia ishu ya kurejea Simba.

“Nafurahi kuwa na mashabiki kutoka Tanzania, nawapenda, kuhusu Simba ni ngumu kulizungumzia ila wakati ukifika itafahamika tu,” alisema Okwi.

SOMA NA HII  MSOLLA: SIJAFIKIRIA KUJIUZULU YANGA