Home Uncategorized SIMBA YAINGIA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA KIFAA KINGINE KIPYA KUTOKA BRAZIL,...

SIMBA YAINGIA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA KIFAA KINGINE KIPYA KUTOKA BRAZIL, KIMECHEZA NA NEYMAR


Mchezaji mwingine kutoka Brazil mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji, Gerson Fraga Vieira (26) amesaini mkataba wa miaka miwili na Simba SC.

Vieira ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 17 ya Brazil iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson.

Feaga pia alicheza timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 20 na alicheza klabu kadhaa za Brazil ikiwepo GrĂªmio amejiunga na klabu yetu akitokea ATK FC ya India.

Usajili umefanyika mara baada ya jana wekundu hao wa Msimbazi kumuongezea mkataba mwingine wa miaka miwili beki wake Mohammed Hussein “Tshabalala”.

SOMA NA HII  COASTAL UNION:BADO TUTAZIDI KUPAMBANA, KESHO WANA KIBARUA MBELE YA KAGERA SUGAR