Home Uncategorized AZAM YAIFANYIA UMAFIA WA AINA YAKE YANGA KWA METACHA

AZAM YAIFANYIA UMAFIA WA AINA YAKE YANGA KWA METACHA


Azam FC imesisitiza kwamba, kipa anayetajwa kumalizana na Yanga, Metacha Mnata, ataitumikia Azam FC msimu ujao na wala haendi sehemu nyingine.

Kauli ya Azam FC imekuja huku kukiwa na taarifa za Yanga kumalizana na kipa huyo ambaye yupo Misri na timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenye michuano ya Afcon.

Metacha ambaye alikuwa kwa mkopo Mbao FC akitokea Azam FC, hivi sasa ni mchezaji huru kutokana na kumaliza mkataba ndani ya Azam FC.

Mtu wa kuaminika kutoka katika ofisi ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, ameliambia Championi kuwa kipa huyo hajasaini kwa mabingwa wa kihistoria Yanga na badala yake ataongeza mkataba wa kuendelea kuwatumika matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam.

“Siyo kweli kuwa Metacha amesaini Yanga, yupo kwenye mipango ya mwalimu na msimu ujao ataendelea kucheza Azam FC kwani ishu ya kumuongezea mkataba mpya tayari imeshafanyika kilichobaki ni kusaini tu,” alisema mtoa taarifa huyo.

SOMA NA HII  BIASHARA UNITED KAMILI KUMALIZANA NA SIMBA