Home Uncategorized WASHINDI 24 WA SMARTPHONE KWENYE USIBAHATISHE CHEZA NA SPORTPESA

WASHINDI 24 WA SMARTPHONE KWENYE USIBAHATISHE CHEZA NA SPORTPESA
Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa Tanzania imewazawadia simu za kisasa za mkononi (smartphone) 24 watanzania mbalimbali walioshinda katika promosheni ya Usibahatishe Cheza na SportPesa.


Washindi hao ni Amran Samwel Mwanga, Jimmy Joseph, Frank Paulo, Juma Issa, Tiblus Dominik, Kassim Mbaga ambao wanatokea Dar es Salaam, Sebastian Mathias, Emmanuel Adebayo (Mwanza), Omary Mohammed, Yahaya Kindenge
(Morogoro), Aliehas Butwah, Yohana Malimi (Geita) na Hawa Ramadhani, Hemed
Mussa (Tanga) na Juma Hamisi kutoka mkoa wa Singida.


Wengine ni Sylvester Myoka (Songea), Raphael Philimon, Festo Mgasa (Arusha), Damian Warwa (Simyu), Lucas Mzalinga (Tabora), Alex Baynic (Dodoma), Anthony Mwembe, Ibrahim Swallo(Njombe) na Jadil Jena anayetokea mkoa wa Mtwara.        


Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa kampuni ya SportPesa Tanzania, Bwana Tarimba Abbas alisema kuwa bado wanaendelea kuwafaidisha Watanzania kupitia mchezo wa kubahatisha kupitia michezo mbalimbali ya kubahatisha
wanayoendesha.


“Huu ni mwendelezo wa promosheni yetu tuliyoizindua wakati wa maandalizi ya ziara ya timu ya Sevilla ya Hispania ambapo mbali ya zawadi za simu, pia tulitoa zawadi za tiketi kwa washindi 45 na kuona mechi ya Simba na Sevilla huku watano wakishinda tiketi za VVIP na kulipiwa malazi, usafiri na chakula siku ya mechi hiyo,” alisema Tarimba.


Pia Bwana Tarimba alisema droo za kuwapata washindi wa Smartphone zinafanyika kila jumatano kwa wiki 15, hivyo kuwa na jumla ya washindi wa Simu janja za kisasa Smartphone 200, tiketi 45 za mechi ya Simba dhidi ya Sevilla FC iliyochezwa tarehe 23 Mei mwaka hu una Sevilla kuibuka na ushindi wa goli 5 kwa 4 na tiketi 10 za mchezo wa Kariobangi Sharks na Everton ya England utakaochezwa nchini Kenya

Julai Mwaka huu. 


Bofya *150*87# kucheza na SportPesa, ni rahisi sana.
SOMA NA HII  BREAKING: SARRI AFUNGASHIWA VIRAGO JUVENTUS