Home Uncategorized ZAHERA AMGOMEA KOCHA MPYA YANGA, AANIKA SABABU ZAKE

ZAHERA AMGOMEA KOCHA MPYA YANGA, AANIKA SABABU ZAKE


KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amegoma katakata kuchaguliwa kocha msaidizi na viongozi wake huku akiwataka wamuachie hiyo kazi yeye wa kuchagua wa kufanya naye kazi.

Zahera ambaye alianza kuinoa Yanga mwishoni mwa msimu wa 2017/18, tangu hapo alikuwa akisaidiwa na Mzania Noel Mwandila ambaye alimkuta kikosini hapo. Yanga hivi karibuni ilihusishwa na mpango wa kuleta kocha msaidizi mpya huku jina la Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime akitajwa.

“Watu wanatakiwa kufahamu kocha Zahera hawezi kuchaguliwa kocha msaidizi wa kufanya naye kazi au viongozi wao wakaniletea, sijui wanichagulie kocha kwa kuwa wanafahamiana naye, hapana.

“Sitaki yanikute yale ambayo yalimkuta kocha wa Simba na msaidizi wake au kule Azam nako ilikuwa hivyo ndiyo maana sitaki kuchaguliwa na tayari tuliongea na mwenyekiti nikamueleza mimi nafanya kazi na kocha Noel na nitaendelea naye na wala sina tatizo naye lolote,” alisema Zahera.

Mapema msimu uliopita, Simba iliachana na Kocha Msaidizi, Masoud Djuma baada ya kutofautiana na Kocha Mkuu Patrick Aussems

SOMA NA HII  MAMBO 7 YANAYOILAZIMISHA ASTON VILLA KUHAKIKISHA INAMPATA NA KUMTUMIA SAMATTA