MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo amesema kuwa harudi Bongo mpaka akaione familia.
Congo imetolewa na Madagascar kwenye michuano ya Afcon hatua ya 16 bora baada ya kupoteza mchezo kwa kufungwa kwa penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya mabao 2-2.
“Tumetolewa kwa penalti hiyo si mbaya sasa ni muda wangu wa kwenda Ulaya kuiona familia maana mwaka mzima nilikuwa na timu yangu ya Yanga hivyo ni muda wangu wa kwenda kupumzika,” amesema.