Home Uncategorized AJIBU KUFURU SIMBA, KULIPWA TSH.MIL 1,250,000 KWA WIKI

AJIBU KUFURU SIMBA, KULIPWA TSH.MIL 1,250,000 KWA WIKI


Lanchi ya juzi haikuwa na raha kwa mashabiki wa Yanga, baada ya Simba kumtambulisha rasmi Ibrahim Ajibu kwamba amerejea Msimbazi.

Simba imemfanyia kufuru nahodha huyo wa Yanga ambapo kila sekunde atakayokuwa akipumua hata kama atakuwa amelala nyumbani kwake watamlipa Sh116. Iko hivi dau lake la usajili alilokunjia mfukoni katika mkataba wa miaka miwili ni Sh.mil 80.

Mshahara wake kwa mwezi ni Sh.mil 5, maana yake ni kwamba kwa mwaka ataingiza Sh.Mil 60. Hiyo inamaanisha pia kwamba kila wiki kwa mshahara huo, Simba itakuwa ikimlipa Sh.Mil 1,250,000 kwa wiki, sawa na Sh 166,700 kwa siku.

Kwa mchanganuo huohuo, Ajibu atakuwa akilipwa Sh 6946 kwa kila saa ndani ya miaka miwili.

Hiyo ni nje ya posho za mechi kama timu ikishinda au kutoa sare na umateumate mwingine wa kishikaji anaopewa na mashabiki.

Mtendaji mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesisitiza kwamba wiki hii ndiyo ya mshtuko mkubwa kwenye usajili wao ingawa hajaweka wazi wanaofuatia.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA ATAJA ILIPOFELI KWENYE PANGA LA NYOTA 14