Home Uncategorized AZAM FC WAANZA KUIWINDA FASIL KENEMA

AZAM FC WAANZA KUIWINDA FASIL KENEMA


ETTINE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya michuano ya kimataifa pamoja na Ligi Kuu Bara.

Azam FC itamenyana na Fasil Kenema kwenye mchezo wa kwanza wa Shirikisho utakaochezwa Agosti 10 nchini Ethiopia.

“Tunajua tuna kazi kubwa kwenye michuano ya kimataifa pamoja na ligi, kwa sasa tumeanza kujiaanda na michuano ya kimataifa na tupo tayari kwa ushindani,” amesema.

 Zimebaki siku 12 kabla ya Azam FC ambao ni mabingwa wa kombe la Shirikisho kuvaana na Fasil Kenema ya Ethiopia.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO