Home Uncategorized JESHI LA SIMBA KUTUA KWA MANDELA

JESHI LA SIMBA KUTUA KWA MANDELA


Kocha wa Simba, Patrick Aussems anatua nchini wiki ijayo na timu inakwenda kambini nchini Afrika Kusini.

Habari za uhakika zinasema kwamba, Simba ilikuwa na mpango wa kwenda Ulaya lakini mpaka sasa wengi wanapendekeza Sauzi ndiyo sehemu nzuri na ina vifaa vyote ambavyo vinastahili kwa kambi ya kiwango cha Simba.

Katibu wa Simba, Dkt Anorld Kashembe alisema mpango wa kambi yao ni kuanza mapema hivyo kwa sasa mipango inaendelea na karibu wataweka wazi kila kitu.

“Kambi inatarajiwa kuanza rasmi kuanzia Julai 15, mwaka huu na tutasema hiyo kambi itakuwa wapi kama ni hapa Bongo au nje ya hapa na lengo ni kufanya maandalizi ya nguvu kama unavyofahamu tuna muda mfupi safari hii tunaingia kwenye ligi huku tukianza michuano ya kimataifa kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.

“Kocha naye ataingia kuanzia Julai 9, lakini siwezi sema siku kamili sababu kunaweza kuwa na mabadiliko ila tutegemee kutua kuanzia wiki ijayo atakuwa hapa kuweka mipango yao kuanzia wiki ijayo,” alisema Kashembe.

Simba ikiwa nchini humo itacheza mechi kadhaa za kirafiki kujiwinda na ligi na michuano ya kimataifa inayoanza Agosti.

SOMA NA HII  AZAM FC YAMALIZANA NA MAJEMBE MAWILI FASTA, MMOJA NI MFUMANIA NYAVU KIMATAIFA