Home Uncategorized KCCA WAAMBIWA NA AZAM FC DAWA YAO ISHAPATIKANA KESHO WANAKALISHWA

KCCA WAAMBIWA NA AZAM FC DAWA YAO ISHAPATIKANA KESHO WANAKALISHWA

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wapinzani wao KCCA kesho wasahau kuwatungua tena kama walivyofanya kwenye mchezo wa awali tayari dawa yao wameshaipata.

Mchezo wa awali Azam FC ilikubali kuchapwa bao 1-0 dhidi ya KCCA ya Uganda kesho watakutana nao kwenye mchezo wa hatua ya fanali kwenye michuano ya Kagame inayofanyika nchini Rwanda.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ettiene Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao ila watawasamehe kesho maana hawana chaguo lingine zaidi ya kushinda.

“Nina amini mechi itakuwa bora zaidi kwa kuwa walitufunga mechi ya kwanza kazi yetu itakuwa ni kulipa kisasi hivyo jambo letu linalokuja ni kupata matokeo hiyo kesho watatusamehe tu kwa kweli,” amesema.

Azam FC ni mabingwa watetezi wa kombe la Kagame walitwaa msimu uliopita uwanja wa Taifa kwa kuiyoosha mabao 2-1 Simba. 

SOMA NA HII  WAZIR JUNIOR AFIKIRIA KIATU CHA UFUNGAJI BORA BAADA YA KUFUNGA BAO LA KWANZA MBELE YA KMC