Home Uncategorized MBAO YATAJA SABABU YA KUFANYA KLINIKI KUSAKA WACHEZAJI

MBAO YATAJA SABABU YA KUFANYA KLINIKI KUSAKA WACHEZAJI


UONGOZI wa Mbao umesema kuwa sababu kubwa ya kufanya kliniki ya kusaka wachezaji ni kutoa fursa kwa wachezaji wanaoipenda Mbao kuitumikia.

Mbao FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Hemed Morroco inaendelea na zoezi la kliniki kwa wachezaji ambalo linafanyika uwanja wa CCM Kirumba.

Katibu wa Mbao FC, Daniel Naila amesema kuwa wanaamini kupitia kliniki hiyo watapata wachezaji wenye vipaji.

“Tunajua kwamba ,Tanzania kuna vipaji na uwezo wa wachezaji ni mkubwa hivyo tumetoa fursa kwa kila anayependa kuitumikia Mbao aonyeshe uwezo wake,” amesema.

Zoezi hilo limeanza Julai 22 majira ya saa mbili kamili linafika tamati leo Julai 24.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA AZAM FC HIKI HAPA, NI MOTO BALAA