Home Uncategorized YANGA WATAJA SIKU YA KUREJEA ZAHERA BONGO

YANGA WATAJA SIKU YA KUREJEA ZAHERA BONGO

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa, Kocha Mkuu Mwinyi Zahera anatarajiwa kujiunga na timu muda wowote kambini Morogoro, kuanzia sasa.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa kwa sasa wanaendelea na mazoezi Morogoro kwa kutumia programu za mwalimu Zahera.

“Kikosi kinafanya mazoezi kwa kutumia programu ya Kocha Mkuu Zahera ambaye anatarajiwa kurejea muda wowote kuanzia sasa,” amesema.

Zahera yupo nchini Ufarasa ambapo alikwenda kwenye mapumziko baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa ya Congo akiwa ni kocha Msaidizi.

SOMA NA HII  MOROCCO KUMSAKA MBADALA WA ADAM SALAMBA