Home Uncategorized MBELGIJI WA SIMBA AJA NA MKAKATI KABAMBE KWA WACHEZAJI

MBELGIJI WA SIMBA AJA NA MKAKATI KABAMBE KWA WACHEZAJI


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa anataka kubadili mfumo kwa wachezaji wake na timu kiujumla kwa ajili ya msimu ujao.

Timu ya Simba imeweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 23 na Simba itafungua ligi kwa kuanza kucheza na JKT Tanzania.

Aussems amesema “Kwasasa nataka kuona wachezaji wakicheza nafasi zaidi ya moja sababu huu msimu nataka kuwa na mifumo miwili au mitatu.

Simba imecheza michezo miwili ya kirafiki na imefanikiwa kupata matokeo chanya ambapo mchezo wa kwanza dhidi ya Orbet TVET walishinda kwa mabao 4-0 na mchez wa pili ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Platinum Stars

SOMA NA HII  PIERRE ASAINI DILI LA MIAKA MITANO TOTTENHAM