Home Uncategorized YANGA YAANDAA GARI MAALUMU LA KUKUSANYA KIJIJI

YANGA YAANDAA GARI MAALUMU LA KUKUSANYA KIJIJI


KATIBU wa Hamasa wa Klabu ya Yanga, Deo Muta amesema kuwa Agosti 4 uwanja wa Taifa lazima wawanyooshe Kariobangi Sharks uwanja wa Taifa.

Yanga itacheza na Kariobangi Sharks kutoka Kenya kwenye siku ya kilele ya cha wiki ya Mwanchi itakayochezwa Uwanja wa Taifa na wameandaa gari maalumu ambalo litapita mitaani kukusanya kijiji.

Muta amesema kuwa gari hilo lipo kwenye hatua za mwisho kukamilika na litapita mtaa kwa mtaa kukusanya kijiji maeneo yote Tanzania.

“Wanayanga wa Dar na Mikoa ya Jirani kaeni mkao chanya wa kukusanyika ili kupata ujumbe kupitia kwa Wasanii mbalimbali watakao kuwa kwenye Gari hilo maalumu na la kisasa ambalo lina Screen kubwa pande zote zitakazokuwa zinaonyesha matukio mbalimbali ya Klabu ya Yanga litakapokuwa linapita Mitaani na Mikoani kwetu.

” Mikoa ya Dar es Salaam Pwani na Morogoro tujitokeze kwa Wingi wakati wa kukusanya kijiji,” amesema.

SOMA NA HII  BREAKING: LIGI KUU BARA, LIGI DARAJA LA KWANZA YASIMAMISHWA KWA MUDA