Home Uncategorized MAANDALIZI STARS YAPAMBA MOTO, AJIBU, MANULA, NYONI NDANI YA KIKOSI

MAANDALIZI STARS YAPAMBA MOTO, AJIBU, MANULA, NYONI NDANI YA KIKOSI



KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa kazi kubwa iliyopo kwa sasa ni kujenga kikosi cha ushindani kitakacholeta matokeo chanya mbele ya Kenya.


Stars ipo kambini na inafanya mazoezi mara mbili kwa siku asbuhi na jioni uwanja wa Bocco kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kufuzu Chan dhidi ya Kenya utakaochezwa Julai 28 uwanja wa Taifa.

Ndayiragije amesema: “Mechi itakuwa ngumu kwa kuwa wapinzani wetu nao wamejiandaa kupata matokeo, kwa sasa tunaendelea kuimarika kidogokidogo na tunawajenga wachezaji kisaikolojia.

“Kwa sasa tayari wachezaji wa Simba wameungana na timu hivyo wataleta fursa ya kuandaa kikosi makini cha ushindani,” ameema.

Wachezaji ambao wamejiunga na timu leo ni pamoja na Aish Manula, Jonas Mkude, Erast Nyoni, Hassan Dilunga, John Bocco, Gadiel Michael na Ibrahim Ajibu.
SOMA NA HII  TPL: YANGA 0-0 AZAM FC