Home Uncategorized MBEYA CITY: TUNAMALIZIA SUALA LA USAJILI

MBEYA CITY: TUNAMALIZIA SUALA LA USAJILI

Mwambusi


JUMA Mwambusi, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa kwa sasa wanakamilisha utaratibu wa mwisho kusajili wachezaji wapya kabla ya dirisha la usjili kufungwa.

Mwambusi amejiunga na timu ya Mbeya City baada ya kupigwa chini na Azam FC msimu uliopita kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuwa na matokeo mabovu.

“Kwa sasa bado tunakamilisha suala la usajili kwa kuwa ni lala salama, utaratibu ukikamilika ndipo tutakuwa huru kuendelea kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

“tunaamini ushindani utakuwa mkubwa ila tupo tayari kwani kila kitu kinakwenda sawa,” amesema.

Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Agosti 31 na Shirikisho la Soka Tanzania limesema kuwa hakutakuwa na muda wa kuongeza.

SOMA NA HII  JESHI KAMILI LA SIMBA LITAKALOANZA LEO DHIDI YA ALLIANCE FC UWANJA WA TAIFA