Home Uncategorized NYOTA WA STARS WAGOMEWA KUSTAAFU NA MWENYEKITI WA HAMASA KWA MTINDO HUU

NYOTA WA STARS WAGOMEWA KUSTAAFU NA MWENYEKITI WA HAMASA KWA MTINDO HUU PAUL Makonda, Mwenyekiti wa Hamasa wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenye michuano ya Afcon amesitisha mipango ya wachezaji wakongwe Kelvin Yondani na Erasto Nyoni kustaafu kuichezea timu hiyo.

Hiyo, ikiwa ni saa chache mara baada ya wachezaji hao kutangaza kustaafu kuichezea stars wakiwa nchini Misri baada ya timu hiyo kuondolewa hatua ya makundi ya Afcon.

Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo, Serena Hotel jijini Dar es Salaam mara baada ya kutua nchini, Makonda amesema kuwa Yondani na Nyoni bado wachezaji na hakuna mchezaji yeyote atakayestaafu kuichezea timu hiyo.


Makonda amesema, kama Kocha Mkuu Mnigeria, Emmanuel Amunike akiwahitaji kwenye kikosi chake, basi ni lazima wote waripoti kambini kama ilivyokuwa zamani. 

“Ninaawambia kuwa ole wenu kocha awaite kwenye kikosi chake halafu simu zenu zisipatikane, basi mtanitambua. 

“Mnatakiwa kufahamu kuwa nyie bado mnahitajika katika timu, hivyo basi Yondani na Nyoni mnatakiwa mlifahamu hilo, tumekuwa kama familia hivi sasa baada ya kuwa pamoja Misri kwenye Afcon,”amesema Makonda.

Aidha Makonda alimuita Yondani kukiri kukubali kubakia stars na kusema kuwa “Nimesitisha mpango wangu wa kustaafu stars, hivyo nitaendelea kuichezea timu yangu.

Kwa upande wa Nyoni alisema kuwa “Nimebaki na nimesitisha mpango wa kustaafu nitaendelea kuitumikia Stars.

SOMA NA HII  DUH!KUMBE ISHU YA KICHUYA NA SIMBA KUNA FILAMU ILIKUWA INACHEZWA