Home Uncategorized SIMBA YAKUBALI KUPIGWA FAINI YA USAJILI

SIMBA YAKUBALI KUPIGWA FAINI YA USAJILI


Wakati usajili wa kimataifa ukifungwa rasmi Julai 10, mwaka huu, Klabu ya Simba imesema haina hofu, ipo tayari kutoa faini ili kuweza kukamilisha usajili wake kwa mchezaji mmoja wa kimataifa ambaye amesalia.

Usajili wa kimataifa, ule wa awali mwisho ilikuwa ni Julai 10, mwaka huu lakini utaendelea mpaka Septemba ambapo ukisajili mchezaji unalipa na faini ya kuchelewa kufanya hivyo.

Mpaka sasa hawa ndiyo wachezaji wa Simba wa kimataifa Meddie Kagere, Claytous Chama, Pascal Wawa, Francis Kahata, Deo Kanda, Gerson Fraga, Wilker Henrique, Sharaf Shiboub na Tairone Santos da Silva.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, alisema kuwa wao kama klabu hawana hofu na suala la faini, cha muhimu ni kupata mchezaji bora ambaye ataisaidia klabu, hivyo watalipa tu.

“Upande wa usajili, sisi kama Simba bado hatujamaliza, sababu kama ule wa kimataifa ulikuwa mwisho Julai 10, lakini baada ya hapo unaendelea mpaka Septemba na sisi tupo tayari kulipa faini ili kuweza kukamilisha usajili wa nafasi moja ya kimataifa ambayo imesalia.

“Ila siwezi kukueleza kuwa ni mchezaji wa nafasi gani ambaye tutamuongeza ila ambua tutamsajili mchezaji mmoja ili kukamilisha usajili na sifa awe mchezaji bora, suala la faini itakuwa kawaida, hakuna namna, sababu tunahitaji kitu kizuri kwa upande wetu.

“Na usajili wa ndani bado, kwa kuwa usajili unafungwa Julai 31, mwaka huu basi tuendelee kusubiri, katika hilo hatuna hofu kabisa,” alisema Magori.

SOMA NA HII  LAMINE MORO ANA KICHWA LAKINI MIGUU IMEMZIDI NGUVU....