TIMU ya Yanga inatarajiwa kucheza na klabu ya Mawenzi Market mchezo wa kirafki katika Tamasha Kubwa la Faith Baptist Church linalotarajiwa kufanyika Julai 28 uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Huu unakuwa ni mwaka wa tano kwa tamasha hilo kufanyika mkoani Morogoro.
Mratibu wa Tamasha hilo, Mchungaji, Jerry Wyatt amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo.
“Kwa miaka minne tumekuwa na mechi kati ya Mtibwa Sugar na Mbeya City lakini mwaka huu wa tano tuna Yanga dhidi ya Mawenzi Market.
“Asubuhi ibada tutafanyia uwanjani hapo na inawezekana mchana tukawa na mechi ndogo ya kirafiki kabla ya Yanga kucheza na Mawenzi Market, tunapenda kutumia mpira kama chombo kuwajenga watu na kuwaweka pamoja na hakuna kiingilio,” amesema.