Home Uncategorized YANGA: MSIMU UJAO MAMBO NI MOTO

YANGA: MSIMU UJAO MAMBO NI MOTO


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa maandalizi ya timu yanazidi kupamba moto kwa ajili ya msimu ujao.

Yanga imeweka kambi mkoani Morogoro ikijipanga kwa ajili ya msimu ujao ambao unatarajiwa kuanza Agosti 23.

Hafidhi Saleh mratibu wa Yanga amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa ni suala la kusubiri wakati wa ligi kuanza.

“Kwa sasa maandalizi yanakwenda vizuri mwalimu Noel Mwandila anawaandaa vijana kwa kutumia programu ya Kocha Mkuu Mwinyi Zahera nina imani msimu ujao tutafanya vizuri kwenye ligi na michuano ya kimataifa,” amesema.

SOMA NA HII  GAKUMBA:KAGERE ATAWAKERA KWELIKWELI