Home Uncategorized YANGA: TUNASHUSHA MUZIKI MNENE KUWAMALIZA WAKALI WA EVERTON

YANGA: TUNASHUSHA MUZIKI MNENE KUWAMALIZA WAKALI WA EVERTON

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa klabu ya Kariobangi Sharks sio nyepesi kwani iliwanyoosha Eveton kutoka England.

Deo Muta, Katibu wa Kamati ya Hamasa amesema kuwa utakuwa ni mchezo wenye ushindani Agosti 4 uwanja wa Taifa siku ya Mwananchi uwanja wa Taifa.

“Everton moja ya klabu bora England wanajua ubora wa Kariobang Shark hivyo nasi tunajua tunakutana na timu ya aina gani kwenye siku ya Mwanachi, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona muziki mnene wa Yanga,” amesema.

Everton ilicheza na Kariobang Shark na kufungwa kwa penalti baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1, mabingwa hao wa kombe la SportPesa watamenyana na Yanga uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  MOLINGA AKUNJA JAMVI LAKE YANGA, KUIBUKIA MOROCCO