Home Uncategorized YANGA: TUNASUKA KIKOSI MATATA

YANGA: TUNASUKA KIKOSI MATATA

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wamejipanga kufanya maajabu msimu ujao hivyo watatumia muda huu wa maandalizi kusuka kikosi imara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kusuka kikosi makini.

“Tunajua msimu ujao utakuwa na ushindani pia tuna kazi ya kufanya kimataifa hivyo tunaandaa kikosi imara cha ushindani,” amesema.

Yanga imeweka kambi Morogoro, ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao na wamecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Tanzanite walishinda mabao 10-1 na dhidi ya Moro Kids walishinda mabao 2-0.

SOMA NA HII  YANGA: MBINU ZA EYMAEL ZIMEJIBU, MASHABIKI WANASTAHILI PONGEZI