Home Uncategorized YANGA WAJIPANGA KUWEKA KAMBI NJE YA NCHI BAADA YA DROO YA CAF

YANGA WAJIPANGA KUWEKA KAMBI NJE YA NCHI BAADA YA DROO YA CAF


FRANK Kamugisha, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano ndani ya Yanga amesema kuwa mpango wa kuweka kambi nje ya nchi haujayeyuka kinachosubiriwa ni droo ya Caf kuchezeshwa kisha watakwea pipa.

Yanga awali ilipanga kuweka kambi nje ya nchi na China ilikwa inatajwa kwa ajili ya matayarisho ya msimu ujao baada ya kukamilisha zoezi la usajili kwa sasa wapo Morogoro.

“Mpango wetu wa kwenda nje upo na tunachosubiri ni kuona ratiba ya Caf itakapotoka tujue tutacheza na timu gani ndipo taamue wapi tunakwenda kuweka kambi.

“Lengo kubwa ni kwenda kuweka kambi nchi itakayokuwa na hali ya hewa na nchi tutakazopangiwa na Caf baada ya droo kuchezeshwa,” amesema.

SOMA NA HII  LIVERPOOL V LEEDS WATAJWA KUWA MCHEZO WENYE USHINDANI EPL