Home Uncategorized ZAHERA ASHINDWE MWENYEWE TU

ZAHERA ASHINDWE MWENYEWE TU


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umefunguka kuwa kwa asilimia 90 umefanikiwa kukamilisha usajili aliokuwa akiutaka Kocha Mwinyi Zahera baada ya kusajiliwa wachezaji aliowapendekeza.

Aidha, kabla ya Zahera kwenda kuitumikia timu yake ya Taifa ya DR Congo katika Michuano ya Afcon 2019, alitoa mapendekezo yake juu ya wachezaji ambao anawahitaji kwa ajili ya msimu ujao jambo ambalo uongozi huo umeeleza kulifanyia kazi.

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alisema kuwa, wanashukuru kuona wamefanikisha kwa asilimia kubwa usajili wa wachezaji aliowahitaji Zahera, hivyo kilichobakia ni maandalizi kwa ajili ya msimu ujao.

“Tumekamilisha matakwa ya kocha lakini suala la kufanya vizuri ama vibaya kwenye ligi ni suala lingine, tunachoangalia hivi sasa ni kukamilisha kile alichokihitaji kocha,” alisema Msolla.

SOMA NA HII  BIASHAA UNITED WANAHITAJI MILIONI 10, HESABU ZAO ZIPO NAMNA HII