Home Uncategorized JUVENTUS, REAL MADRID WAPIGANA VIKUMBO KUINASA SAINI YA POGBA

JUVENTUS, REAL MADRID WAPIGANA VIKUMBO KUINASA SAINI YA POGBA


REAL Madrid imeweka mezani pauni milioni 27.6 pamoja na nyota wao James Rodriguez ili kumpata kiungo wao Paul Pogba dili ambalo inaelezwa lilipigwa chini na mabosi wa United.

Sasa, Juventus imeamua sasa kuweka wachezaji wake watatu ili kumpata nyota huyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Ripoti zinaeleza kuwa Juventus wamemtuma kiongozi wa idara ya michezo Fabio Paratici, Makamu Mwenyekiti, Pavel Nedved na wakala matata Mino Raiola England ili kukamilisha dili hilo.

Juventus ipo tayari kumuachia Paulo Dybala, Mario Mandzukic na Blaise Matuidi ndani ya Old Trafford ili kuipata saini ya Pogba.

SOMA NA HII  KMC WANA BALAA, WATIA TIMU LEO RWANDA NA KUANZA KUWAVUTIA KASI WAPINZANI WAO