Home Uncategorized MAANDALIZI NDANI YA SINGIDA UNITED YAMEPAMBA MOTO

MAANDALIZI NDANI YA SINGIDA UNITED YAMEPAMBA MOTO


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa kwa sasa unaendelea na maandalizi ya nguvu kuelekea msimu ujao.

Singida United imejichimbia Singida kwa sasa kwa maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 23.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa kikosi kipo sawa kwa ajili ya msimu ujao na maandalizi yaaendelea.

“Kwa sasa kikosi kipo kambini na maandalizi kwa ajili ya msimu ujao yanaendelea, matumaini yetu ni kufanya vizuri.

“Wachezaji wetu wapo vema wanasubiri masaa ya kuanza kuonyesha maajabu kwa kile amabacho wamejiifunza,” amesema.

SOMA NA HII  SAKATA LA MORRISON LAIBUKA UPYA KABISA