Home Uncategorized MBAO WAPO VIZURI, KUANZA KAZI NA AALIANCE FC

MBAO WAPO VIZURI, KUANZA KAZI NA AALIANCE FC


UONGOZI wa Mbao FC umesema kuwa umekamilisha mipango kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 24.

Mbao FC kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu, Hemed Morroco baada ya kuachana na Salum Mayanga ambaye ametua Ruvu Shooting.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi amesema wamejipanga kiasi cha kutosha kuleta ushindani. 


“Kikosi kipo salama na kinaendelea kukamilisha maandalizi ya mwisho, tunajua kwamba mashabiki wanahitaji burudani nasi tunachofanya ni kuandaa mipango makini.

 “Muda wetu wa kufanya vema ni sasa kwani tunaanza na ndugu zetu Alliance lazima tufanye kweli,” amesema.

Mchezo wa Kwanza kwa Mbao utakuwa dhidi ya Alliance utachezwa Uwanja wa Kirumba Agosti 24 na Alliance atakuwa mgeni.

SOMA NA HII  NYOTA WA SIMBA NA YANGA AJIUNGA NA TIMU YA PRO LINE