Home Uncategorized MBELGIJI SIMBA AWAGOMEA WABRAZIL

MBELGIJI SIMBA AWAGOMEA WABRAZIL


KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick aussems amesema haoni nafasi ya wachezaji wake watatu kutoka Brazil kupata namba za kudumu kwenye timu hiyo kutokana na viwango vyao ikiwemo suala la kuzoea mazingira.

Simba imesajili nyota watatu kutoka nchini Brazil kwa ajili ya msimu jao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo imeshaanza.

Wachezaji hao walisajiliwa na Simba kutoka Brazil ni mabeki Gérson Fraga Vieira kutoka Atletico De Kolkata ya India, Tairone Santos da Silva (Atlético Cearense, Brazil) na mshambuliaji Wilker Henrique da Silva aliyekuwa UA Barbarense ya Brazil.

Aussems alisema kuwa, hategemei kuwatumia kucheza mechi nyingi sana wachezaji hao kwa kuwa wanahitaji muda wa kutosha kutokana na suala la viwango vyao.

“Binafsi sikuwa na mpango wa kuhitaji mchezaji yoyote kutoka Brazil lakini nimekuta wamesajiliwa na uongozi ila ukweli mpango wangu haukuwa wa namna hiyo.

“Nadhani suala la wao kuwatumia katika kila mechi binafsi kwa sasa halipo lakini wanaweza wakawa wanacheza mechi mbili, tatu ila siyo kuamini ndiyo watakuwa kila kitu kwa sasa kwa sababu bado wanahitaji muda wa kutosha kwa kujua mambo mengi,” alisema Aussems.

SOMA NA HII  MIDO HATARI BONGO AKUBALI KUTUA YANGA, ISHU YA SVEN KUPEWA MECHI TATU IPO HIVI, NDANI YA SPOTI XTRA