Home Uncategorized MSEMAJI WA YANGA MPYA YANGA APATIKANA

MSEMAJI WA YANGA MPYA YANGA APATIKANA


Tunaweza kusema kuwa kile kilio cha mashabiki na wanachama wengi wa Yanga kutaka Dismas Ten aondolewe katika nafasi ya usemaji na badala yake atafutwe mtu mwingine inaweza kuwa imepatikana.

Taarifa zinasema kuwa mwanachama na shabiki wa Yanga, Antonio Nugaz, ambaye pia ni mtangazaji katika kituo cha Clouds Media Group, anatajwa kuchukua nafasi ya Dismas Ten.


Nugaz ambaye amekuwa akijitahidi kuhudhuria mechi nyingi za Yanga, leo ameonekana akiwa na Dismas Ten ambaye alikuwa kwenye nafasi hiyo.

Taarifa zilizo ndani ya Yanga zinasema kuwa Nugaz anaweza akatangazwa muda wowote kuanzia sasa kurithi nafasi hiyo iliyopooza kama mashabiki wengi wa Yanga wanavyosema.


SOMA NA HII  KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA KIAKACHOANZA LEO DHIDI YA KENYA, UWANJA WA TAIFA