Home Uncategorized NYOTA MPYA WA YANGA, RAIA WA RWANDA SIBOMANA AAMUA KUFANYA KWELI, AMSHUSHA...

NYOTA MPYA WA YANGA, RAIA WA RWANDA SIBOMANA AAMUA KUFANYA KWELI, AMSHUSHA MKEWE DAR


PATRICK Sibomana, mshambuliaji mpya wa Yanga ameamua kufanya kweli kwenye mchezo wa kimataifa wa kesho dhidi ya Townshipp Rollers.

Muda mfupi kabla ya kuwavaa wababe hao mke wake kipenzi ametia timu Dar ili kumuongezea nguvu ya kufanya kazi kwa umakini.

Habari zinaeleza kuwa lengo kubwa la nyota huyo raia wa Rwanda kumleta mke wake huyo ni kupata tiba ya msosi ambao anaupenda akiwa Rwanda kabla ya kuwavaa wapinzani wao kesho.

Tayari Sibomana ameanza kuonyesha makeke kwenye mechi za kimataifa kwani kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Kariobangi Sharks alipachika bao moja kwa mkwaju wa penalti jambo linaloonekana ni nyota njema kwakwe na wana Yanga kiujumla.

SOMA NA HII  HIKI HAPA ANACHOKIFANYA ABDI BANDA KULINDA KIPAJI CHAKE